THE LUTHERAN RADIO CENTRE

 

 ANNOUNCEMENTS:

 

 

  PRAYER REQUESTS   LUTHEAN RADIO CENTRE:

KUPANDA KWA GHARAMA ZA LESENI YA UTANGAZAJI GHAFLA

Msikilizaji mpendwa Kutokana na kupanda kwa gharama za leseni ya utangazaji ya kutuwezesha kurusha matangazo ya Redio Sauti ya Injili sehemu mbalimbali kutoka kiwango cha shilingi milioni 36 kwa mwaka hadi shilingi milioni 60 ambayo inatakiwa kulipwa kwa haraka ili tuendelee kusikika hewani.

Msikilizaji mpendwa wa Radio Sauti ya Injili kutokana na gharama hizo kupanda kwa ghafla na kufikia shilingi milioni 60 ili Sauti ya Injili iendelee kusikika hewani tunaomba mchango wako wa kiasi chochote kwa kadri Mungu alivyokujalia ili tuweze kulipa gharama hizi za leseni na kuendelea kusikika hewani.

Endapo hatutalipa kiasi hicho kwa wakati tutatakiwa kulipa faini kila mwezi asilimia kumi na tano, ya milioni sitini.

Redio Sauti ya Injili Moshi ina mitambo maeneo mbalimbali kama vile, Arusha, Kibaya, Moshi, Rombo, Same, Usambara,Tanga,Morogogoro na Ngorongoro ambayo hutumika kukufikishia matangazo ya Radio Sauti ya Injili katika maeneo yako.

Hivyo basi msikilizaji mpendwa tunaomba mchango wako wa hali na mali ili kuweza kufanikisha malipo ya leseni.

Mchango wako unaweza kuutuma kwa Mpesa namba 0758922922 au Tigo pesa 0655922922 au kupitia benki

Uchumi Commercial Bank A/C.No. 00101010539 Au

National Bank of Commerce (NBC) A/C. No. 017101001820 Moshi Branch

Au unaweza kufika Redio Sauti ya Injili ofisi ya Mkurugenzi.


Uongozi pamoja na watumishi wa Redio Sauti ya Injili tunapenda kuendelea kukuhudumia vizuri kila siku.

Ahsante kwa ushirikiano wako wa kuendelea kuibeba Redio yako Sauti ya Injili (Kristo kwa mataifa yote) Mungu akubariki.

KWA MAOMBI AU USHAURI WA KIROHO WASILIANA NA MTUMISHI WA MUNGU EZRA JOHN:  

kwa simu Namba: 0754518757 au 0658528757.

 

 

 Announcement 1

 

 Announcement 2
Important Links:    ELCT   LRC Mirror site Tansania   LRC ELCT LRC Backupserver   LWF   RADIO UPENDO DAR   RADIO FURAHA   TWR   Habari Maalum
                                    All Rights Reserved 2019